Wednesday, August 28, 2013

ALIYEMCHANA KWA CHUPA AUNT EZEKIEL NI HUYU HAPA.


Mwanamke mmoja amabye amejulikana kwa jina moja tu la Yvonne ndiye anayedaiwa kumchana kwa chupa muigizaji Aunt Ezekiel juzi usiku katika Club Billicanas. Inadaiwa siku za nyuma Aunt Ezekiel aliwahi kumchukulia Yvonne mwanaume wake na waliingia katika mzozo hivyo inawezekana Yvonne amelipiza kisasi ingawa Aunt alisema walishayamaliza. Yvonne alitaka kumpiga chupa ya uso Aunt sema akaiwahi kuizuia kwa mkono na ndiyo ikamchana. akizungumza na paparazi wa GPL alisema...........

KAGAME AKATA MGUU TANZANIA

Banner

RAIS Paul Kagame wa Rwanda, sasa hayupo tayari kukanyaga ardhi ya Tanzania kutokana na kile kinachoonekana kuwa ni mgogoro wa kidiplomasia unaoendelea kati yake na Rais Jakaya Kikwete. MTANZANIA Jumatano limedokezwa.

Wakati hayo yakifikia hapo, kikao cha Bunge la Afrika Mashariki (EALA), linakoketi mjini Arusha kilivunjika baada ya Spika wa bunge hilo, Magreth Zziwa, kugongana kauli na Mbunge mmoja wa Rwanda jambo lililosababisha wabunge wote wa Rwanda kususia kikao na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge. 

Tuesday, August 20, 2013

MAANDAMANO YA CHADEMA KUMNG'OA MEYA ILEMELA JIJINI MWANZA YAISHA KWA MABOMUMAANDAMANO ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) yamegeuka shubiri kwa wakazi wa jiji la Mwanza baada ya kuibuka mapambano makali baina ya waandamanaji hao na jeshi la polisi mkoani Mwanza na kusababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa chama hicho.Maandamano hayo ya amani ambayo yalianzia katika eneo la Buzuruga nje kidogo ya jiji la Mwanza yalikuw ayakiongozwa na wabunge Highness Kiwia wa Ilemela pamoja na Ezekiel Wenje kuelekea katika viwanja vya Furahisha yalilenga kumshinikiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo kutoa barua zinazodaiwa kuandikwa na ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi kuwarejesha madiwani watatu waliotimuliwa katika Manispaa ya Ilemela kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo.Polisi wenye silaha pamoja na askari kanzu walianza kutanda katika eneo hilo la Furahisha wakiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza RCO Konyo ambaye alikuwa akitumia gari lenye namba za usajili DK 068EXV aina ya Toyota Land Cruiser

Maandamano yakipita barabara ya Balewa kuelekea barabara ya Makongoro hatimaye viwanja vya Furahisha Kirumba Mwanza.


Mtaa wa jiwe kuu kata ya Kitangiri na ujumbe wao.


Maandamano hayo ambayo awali yalionekana kana kwamba yangelimalizika salama yaliwasili katika viwanja vya Furahisha majira ya saa 5.38 huku yakiongozwa na gari la polisi lenye namba za usajili za nchi ya Uganda 779 UAG likiwa nimesheheni polisi wenye silaha nzito ikiwa ni pamoja na mabomu ya machozi na bunduki pamoja na askari kadhaa ambao walikuwa katikati ya maandamano hayo.


Askari polisi akiwaelekeza waandamanaji njia ya kuingia viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.


Walioacha shughuli zao za kila siku waliungana na wale ambao walikuwa shughulini kutafuta kipato kama mama huyu mstari wa mbele kwenye maandamano.
Baada ya maandamano hayo kuwasili katika viwanja vya Furahisha kwa amani,waandamani hao ambao walikuwa na mabango mbalimbali yaliyosomeka kuwa ‘Matata hatutaki uendelee kuwa Meya wa Ilemela rudia kazi yako ya awali, na jingine Jaji Sumari tumechoka kuahirisha mara kw amara kesi dhidi ya Matata na jingine lililosomeka kuwa RD Ndikilo tunahitaji barua za kurejeshwa kwa madiwani wetu.


Hata hivyo tofauti na ilivyokuwa imetangazwa kuwa maandamano hayo ya amani yangelipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo,hakukuwa na kiongozi yoyote wa Serikali ambaye alikuwepo uwanjani hapo kupokea maandamano hayo.Kufuatia kutoonekana kwa kiongozi yoyote wa Serikali,viongozi wa chadema pamoja na wabunge wao walikutana kwa faragha kwa dakika kadhaa kwa ajili ya kujua hatima ya maandamano hayo ambapo Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje alipanda jukwaani saa 6.45 na kuwaeleza maelfu ya waandamanaji kuwa wameamua kumtuma Mbunge wa Ilemela Highnes Kiwia kwenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuchukua majibu kwa ajili ya kuwaletea wananchi walioandamana juu ya hatima ya madiwani hao.

Chanzo:>GSengo

Sheikh Ponda Mtuhumiwa ghali zaidi

Inasemwa kwamba...
*Arushwa kwa helikopta hadi Morogoro
*Asomewa mashitaka ya uchochezi
KATIBU wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda (54) jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Morogoro akiwa chini ya ulinzi mkali baada ya kuwasili katika uwanja wa Gofu mjini Morogoro kwa helikopta ya polisi. Ponda alifikishwa mahakamani Morogoro,
baada ya mapema asubuhi jana kuachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa shtaka la kuhamasisha wafuasi wake kufanya fujo, kabla ya kukamatwa tena na polisi.

Akisoma mashitaka matatu dhidi ya Sheikh Ponda mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Morogoro Richard Kabate, Mwanasheria wa Serikali, Bernard Kongola akiwa na wanasheria wenzake wa serikali, Gloria Rwakibalira na Akisa Mhando, alidai Agosti 10 mwaka huu katika eneo la Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro, Ponda alitoa maneno ya uchochezi.

GAZETI MAWIO LEO MITAANI, LADAIWA KUCHUKULIWA NA MWANAHALISI

13 548e9

Monday, August 19, 2013

Wafuasi wa Ponda wapiga kambi SegereaOfisa Habari wa Magereza, Deodatus Kizinja alisema kisheria ni watu wawili tu kwa mwezi wanaoruhusiwa kumwona mahabusu mmoja.
Dar es Salaam.

Saturday, August 17, 2013

ARSENAL YAANZA VIBAYA
 306552hp2
Msimu wa Ligi Kuu ya soka ya England umeanza kwa kishindo kwa Aston Villa kuwashtua Arsenal kwa mabao 3-1 katika uwanja wa Emirates.

MAJAMBAZI WAWILI WAUWAWA NA WANANCHI JIJINI MWANZAWATU wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa na wananchi mkoani Mwanza wakati wakijaribu kuiba katika kituo cha mafuta cha GBP.

Akizungunzumza na mwandishi wetu, shuhuda mmoja ambaye alikuwa eneo la tukio hilo alisema kuwa majambazi hao walifika katika kituo hicho cha mafuta wakitaka kuiba

LIGI KUU UINGEREZA KUANZA KUTIMUA VUMBI LEOLigi ya Uingereza yenye mashabiki wengi duniani na inayofuatiliwa kwa karibu sana hapa kwetu Tanzania,inaendelea leo.
Timu nyingi zitakua viwanjani kutafuta matokeo mazuri huku ligi ikiwa inaenda ukingoni,baadhi ya timu zinahitaji matokeo mazuri ili kumaliza nafasi bora za juu wakati nyingine zikijaribu kujinasua na hatari ya kushuka daraja.
Mechi za leo jumamosi:Friday, August 16, 2013

TASWIRA YA MASHINDANO YA DANSI FIESTA KIGOMA 2013

Maoni mbalimbali yasikika kuhusu makundi yaliyochaguliwa kushiriki shindano hilo.

Mwanadada mwenyeji wa Kigoma mjini akitoa maoni yake kuhusu makundi yaliyoshiriki Dansi La Fiesta 2013 siku ya Alhamisi 17 August 2013 ndani ya club Lake View Kigoma mjini.

Alex Mzambele akiwa na Adam Mchomvu wakitangaza washindi wa Dansi La Fiesta usiku wa Alhamisi 15 August ndani ya club ya Lake View Kigoma mjini.

"KIAMA CHA WASANII MAMISS KIMETIMIA.....FANI IMEWASHINDA NA WAMEKIMBILIA KUJIUZA"...


BAADA ya wasanii waliotoka kwenye mashindano ya u-miss kuvuma sana na 
kupotea ghafla, msanii mkongwe kunako gemu la filamu Bongo, Salome 
Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ amefunguka na kudai 

Hit list ya Fiesta Kigoma yatembelea kaburi la Ngwear kabla ya safari


Wasanii wa Bongo fleva watembelea kaburi la marehemu Albert Mangwea,(Kihonda) Mjini Morogoro asubuhi ya leo na kumuombea dua pale walipokuwa wakipita kuelekea mkoani Kigoma

Wednesday, August 14, 2013

Yanga noma, yaibwaga Simba vita ya Ngasa

KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) inakutana kwa siku mbili kuanzia kesho Jumatano kujadili utata na pingamizi za usajili wa wachezaji wa Ligi Kuu Bara, lakini Yanga inaonekana kuwa na faida zaidi kuliko Simba kuhusu suala la Mrisho Ngassa.