Friday, August 16, 2013

"KIAMA CHA WASANII MAMISS KIMETIMIA.....FANI IMEWASHINDA NA WAMEKIMBILIA KUJIUZA"...


BAADA ya wasanii waliotoka kwenye mashindano ya u-miss kuvuma sana na 
kupotea ghafla, msanii mkongwe kunako gemu la filamu Bongo, Salome 
Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ amefunguka na kudai utabiri wake umetimia. 
 
Akizungumza na mwandishi  wetu hivi karibuni, Thea alisema miaka kadhaa iliyopita 
alitabiri kuwa wasanii waliokuwa wanavuma sana ambao walitokea kwenye 
mashindano ya u-miss, hawatadumu kwenye uigizaji hivyo utabiri wake 
umetimia kwani sasa hivi, hawavumi tena.
 
“Utabiri wangu unafanya kazi kwa sababu kwa sasa wale wasanii walioibukia kwenye mashindano ya 
u-miss wengi hawasikiki tena, wasanii wanatakiwa kutambua kuwa sanaa hii
 siyo lelemama yaani mpaka kufikia hapa tulipo tulifanya kazi ya ziada, 
tulisota sana kwenye vikundi,” alisema Thea

No comments:

Post a Comment