Sunday, September 15, 2013

JESHI LA RWANDA LAELEKEZWA CONGO

Vikosi vyake vyasogezwa mstari wa mbele
*SADC yakaa chonjo, yaionya tena Kigali

VIKOSI vya wanajeshi vya Serikali ya Rwanda vyenye silaha za kivita, sasa vimesogezwa katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Taarifa ya kusogezwa kwa vikosi hivyo mstari wa mbele katika eneo la mpakani, imetolewa jana na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).